NB: USAFIRI BURE MIKOA YOTE YA TANZANIA
JINA KITABU: MWANDAE MTOTO WA KIUME KUWA MWANAUME
JINA LA MWANDISHI: HANIFA KAFASHE
MWAKA WA UCHAPISHAJI TOLEO LA 1: 2025
KUHUSU KITABU
MALEZI ni wajibu usio na kikomo ambao binadamu humsaidia mwingine kujitambua na kukua kiakili katika maisha. Kitabu cha *Mwandae Mtoto wa Kiume kuwa Mwanaume* kimejikita katika falsafa ya malezi ambayo inawezesha kumjenga mtoto wa kiume. Katika falsafa ya malezi ni muhimu Mzazi au Mlezi kuchagua njia bora za kumtengeneza mtoto wa kiume kuwa mwanaume bora. Kitabu pia kinaangazia namna ya kumlinda katika usalama, kumwezesha kiuchumi, kumshauri, kumwelimisha na kumkuza kihisia na kimwili. Kumwezesha kuyaelewa mazingira yake, uhusiano na watu, mabadiliko ya mwili wake, matamanio yake, ndoto zake, njia zake, kipaji chake, shujaa wake na namna bora ambayo mzazi au Mlezi angependa kuona mtoto wake wa kiume anakuwa sehemu ya jamii bora. Kama tujuavyo, malezi si kazi ya watu wavivu wala si lelemama bali inahitaji kuvumilia, kuelekeza, kupenda na kuzingatia njia sahihi za kumkuza.
Vilevile kitabu kinaweka misingi kwa wazazi na Walezi katika jukumu lao la kuwafundisha watoto wa kiume mbinu mbalimbali za maisha zenye mguso wa kipekee.
Hayo na mengine mengi utayasoma kitabuni humu.
HANIFA KAFASHE